Thursday, 7 April 2016

MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI YA TAGAMENDA YASIYOTUMIKA KWA SASA

Moja ya bweni la shule ya sekondari ya Tagamenda lisilotumika kwa sasa likisubili mpango wa kuanzishwa kidato cha tano ambao ulitakiwa uwe umeshaanza miaka miwili iliyopita. Mwaka jana lilikuwa likitumika na wanafunzi wa madarasa ya mitihani hasa kidato cha nne ila kwa sasa uendeshaji hosteli hii  umekwama kutokana na mpango wa serikali wa elimu bure kwani awali wazazi walikuwa wakichangia gharama za chakula, umeme na maji suala amabalo kwa sasa limekuwa gumu kulitekeleza.

Jengo la bweni la shule ya sekondari Tagamenda lililoanza kujengwa  miaka mitano iliyopita kwa nguvu za wananchi amabao walijitolea tofari, mawe, mchanga, bati , nguvu pamoja na vifaa vingine. Umalizia wake umekwama na kupelekea kuendelea kuchaka bila kutumika, jengo hili endapo lingemalizika lingeweza kuwasaidia wanafunzi wa vidato vya mitihani na wale wanaoishi mbali na shule.

No comments:

Post a Comment